Friday, 13 September 2013

TAARIFA YA UTAMBULISHO NA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA SHIRIKA LA WEZESHA WAKULIMA TANZANIA (TANZANIA FARMERS EMPOWERMENT,TAFE ) KWA WANANCHI WA WILAYA YA NANYUMBU- MTWARA




Shirika la WEZESHA WAKULIMA TANZANIA (TANZANIA FARMERMES EMPOWERMENT)- (TAFE) ni asasi isiyokuwa ya kisiasa, kidini,kikabila na kifaida ilianzishwa tarehe 22/3/2013 ikisajiliwa rasmi kuwa kikundi jamii (COMMUNITY BASED ORGANIZATION) (CBO) kwa namba MTW/NANY/KU 197, ni shirika linaloongozwa na vijana 19 waliohitimu elimu ya chuo kikuu kutoka katika chuo kikuu cha Dodoma kwa shahada mbalimbali na pia wanafunzi kutoka katika chuo cha kilimo cha Sokoine (SUA). Hii ni pamoja na kutambua changamoto mbalimbali ambazo zinaikumba jamii yetu ya Tanzania kwa sasa hasa tatizo la elimu na Ajira.
Hivyo kwa kushirikiana na serikali,taasisi zisizo za kisekali pamoja na mashirika mengine ya maendeleo wakiwemo wanaharakati wengine wa maendeleo Wezesha wakulima Tanzania inaamini Maendeleo ya Tanzania  yatafikiwa kupitia mipango yake ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Malengo ya Millenia 2015 na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania pamoja na mikakati Mingineyo mbalimbali.
Makao Makuu ya Shirika ni Katika Kijiji cha Lumesule, Kata ya Lumesule Wilayani Nanyumbu ambako shirika linashirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhakikisha malengo haya yanafikiwa.
Katika kuhakikisha kwamba shirika linafikia malengo yake ni wazi kwamba kulikuwa na kila sababu ya kijuitambulisha kwa wananchi ili jamii itoe ushirikiano wa kutosha kwao, kwa kuzingatia hili shirika liliandaa vikao mbalimbali ili kuhakikisha ushawishi mkubwa unafanywa kwa wananchi kukubali mradi huu muhimu kwa maendeleo ya mkulima mwenyewe. Shirika lilifanya Vikao mbali mbali pamoja na jamii ili kufanikisha lengo hili la ushawishi kwa jamii kukubali kushirikiana na jamii husika

UTAMBULISHO .
Utambulisho ulikuwa wa aina mbili ambao ni shirika pamoja na uongozi wa vijiji vyote vilivyohudhuria kikao hiki cha mafanikio ya wakulima.  Wajumbe waliohudhuria kikao pia walipata nafasi ya kujitambulisha mmoja mmoja kwa mujibu wa mwenyekiti wa kikao nafasi zao katika utumishi.
Utambulisho wa shirika la WEZESHA WAKULIMA TANZANIA (TAFE) ulipelekwa moja kwa moja kwa Katibu Mtendaji wa shirika ambaye ni REV.Linus John Buriani. Alianza kwa kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wa shirika ambao waliweza kufika katika kikao hicho ambapo alitoa hudhuru wa baadhi ya wanachama wengine wa shirika kutowezakufika kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo ile yawengine kuwepo katika Jukwaa la Vijana la Katiba lililofanyika Dar es salaam. Wajumbe wa shirika walioweza kufika walikuwa wajumbe wanne akiwemo
Mratibu washirika kanda ya Kusini ndg. Steven Namahochi
Mratibu wa shirika kanda ya kaskazini ndg.John Thomas pamoja na
Afisa msaidizi mawasiliano ndg Sharifu Muibu.
Wakiongozwa na Katibu Mtendaji Rev. Linus John Buriani ambaye kwa mujibu wa Katiba yeye ni Mratibu Mkuu wa Shirika  huku akiutambulisha na uongozi mzima wa shirika akiwemo ndg Victor Willium kama mwenyekiti wa shirika ,Miss Victoria mponda kama mtunza hazina wa shirika.Na pia walitajwa viongozi wengine ambao hawakuwepo kama Mratibu wa kanda ya Mashariki Bi, Barka Omari pamoja na Mratibu wa kanda ya Kusini Nyanda za Juu Bi, Sarah Kazumba na Afisa Habari,Technologia na Mawasiliano Bwana George makona kutoka Mbeya.
Mgeni rasmi ambae ni Mh Mbunge wa jimbo la Nanyumbu naye alijitambulisha yeye na ujumbe wake wote ambao alikuja nao katika kikao hicho cha Utambulisho.
Katibu Mtendaji alitoa maelezo machache sana ambayo yaliifanya kikao cha maamuzi cha shirika kufikia kulipeleka shirika lumesule na hasa katika Wilaya ya Naunyumbu na moja kati ya sababu Katibu aliitoa ni pamoja na:

Tatizo la ajira kwa vijana
 Katibu alichukulia mfano wa vijana wengi katika kijiji cha Lumesule kutwa kukaa bila kitu cha kufanya huku akizidi kuzungumzia mzigo mzito wa serikali juu ya ajira kwa vijana ukiongezeka siku hadi siku.”…asilimia ya vijana Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa ni  66% ya watu wote Tanzania huku ikisemekana kwamba mnamo mwaka 2050 Tanzania itakuwa ni nchi ya 3 barani Africa kuwa na idadi kubwa ya watu ambao ni vijana” Hivyo basi kwa kutambua changamoto la ukuaji wa idadi ya watu na kasi ya ukuaji wa Uchumi shirika likaona iko haja ya kwenda kuweka makao makuu yake katika Wilaya ya Nanyumbu ambako kasi ya ukuaji wa uchumi  ni ndogo ukizingatia na kasi ya ukuaji wa kundi la vijana ambalo halina Ajira na elimu ya kujitegemea. “Bila shaka sisi tunaamini Tanzania ni nchi ya Kilimo na ili uchumi ukue kwa kasi kubwa ni lazima macho makali yaelekezwe kwenye sekta ya kilimo ambako hutoa ajira kwa watu wengi na mahitaji muhimu kwa jamii.” ( Rev. Linus John Buriani, Katibu mtendaji wa shirika)

MALENGO YA SHIRIKA
Malengo ya Shirika ni pamoja na kufanya mabo yafuatayo.

Mafunzo ya ujasiriamali (entrepreneurship) 
Sababu nyingine iliyopelekea kuanzishwa kwa shirika katika wilaya ya nanyumbu ni nia la kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kumwezesha mkulima na mwanakijiji wa leo kutotegemea kitu kimoja katika kuendelea na haswa ikiwalenga vijana.Vijana wengi wamalizapo elimu yao ya kidato cha nne wengi wao wanapokosa nafasi ya kuendelea mbele hiushia magengeni na wengine katika mambo hatarishi ya maisha yao wakikusudiakuifurahisha mioyo yao wasijue ni kujiumiza. Shirika limeandaa mpango wa kuwapa mafunzo vijana ambao wamekata tama na maisha juu ya ujasiriamali na maendeleo ili kuepusha uzururaji na utumiaji wa madawa ya kuelvya kwa vijana.

Jinsia ( gender )
Katika jamii inayotuzunguka ya leo kati ya mambo yanayokwamisha maendeleo ya mkulima ni utofauti uliopo kati ya jinsia mbili ya (me) na (ke). Baadhi ya jamii nyingi Tanzania swala la maendeleo linamgandamiza mwanamke kuliko mwanamume huku hii ikididimiza uwezo wa wanawake katika maendeleo na mwisho kukwamisha maendeleo ya kujikimu. Shirika limeandaa mipango mikakati mbadala katika kuondoa utofauti uliopo haswa katika kilimo. Tanzania inategemea kilimo ili kuongeza uchumi wake na wa watu wake lakini kiwango shirikishi katika uzalishaji kinamgandamiza mwanamke huku mwanamume akizidi kukiona kilimo kama kazi ya mwanamke. Ushirikishwaji na usawa katika kilimo unafanya ufanisi katika maendeleo na hivyo shirika limejiandaa kutoa mafunzo kwa jinsia mbili na nafasi zao katika maendeleo ya kilimo Tanzania.

Utafiti (research)
Shirika pia limeanzishwa kwa nia na kusudi la kufanya uchunguzi wa namna ya kuboresha kilimo nchini Tanzania na haswa ikianzia katika mkoa wa Mtwara.utafiti utaambatana na kumnufaisha mkulima na kuleta tija katika maendeleo. Mkulima wa sasa analima kwa mazoea pasipokujua utaalam wa kilimo kwa kushirikiana na serikali shirika limeanda mpango wa kufaanya utafiti wa mazao na njia mbalimbali za kumwezesha mkulima kulima kukiwa na tija kwenye maendeleo.

Ushirikiano(partnership)
Ushirikiano huu utalenga serikali,mashirika binafsi,taasisi za dini na mashirika ya kimataifa. Ili kuboresha kilimo cha mtanzania wa sasa kushirikiana na serikali katika mpango wa kukuza na kuondoa umaskini tanzana (MKUKUTA) ya mwaka 2015 pamoja na mpango wa maendeleo (TANZANIA DEVELOPMENT VISION)(MKUZA) 2025 tumenuia kushirikiana kwa hali ya juu kwa zileshemu zisikofikiwa na serikali kwa urahisi kuhakikisha zinafikiwa kwa ushirikiana kati ya shirika na Halmashauri wilya,mkoa naa wizara husika katika kilimo, maendeleo,vijana nyingine husika. Ushirikiano pia umekusudiwa kati ya shirika na mashirika ya kimataifa ikiwa ni pamoja na shirika la maendeleo duniani na asasi ndogondogo za umoja wa kimataifa katika kupambana na umaskini duniani katika mpango wa millennia(2000).

Elimu ya rika(elimu rika)
Elimu hii ikiwagusa vijana katika mabadiliko ya tabia na namna ya kukabiliana nazo wakati zinapoonekana tabia kama hizo. Hii itasaidia kuondoa mimba za utotoni na zaidi kumsaidia kijana kupambana na mazingira ya nayomzunguka.

MIKAKATI YA SHIRIKA
Katibu pia katika kulitambiulisha shirika aligusia mikakati madhubuti ikiwemo ya muda mfupi na muda mrefu ndani ya shirika.

Mikakati ya muda mfupi :( short term strategies)
Kutengeneza vikundi vya wakulima; shirika limekusudia njia ya kwanza ya kumnufahisha mkulimaa katika wilaya ya nanyumbu kwanza kutengeneza vikundi vya wakulima ambapo shirika limekusudia kuwa na vikundi vipatavyo 21 katika kila kijiji.
Kuanzisha mashamba darasa kwa ajili ya mafunzo ya wakulima ambapo wataalam wa maendeleo kutoka katika shirika na vyuo vya kilimo na pia maafisa kilimo kutoka serikalini wataandaa mafunzo rasmi kwa wakulima kulingana na uhitaji halisi wa wakuliuma katika vikundi.
Utafiti tathmini (baseline surveying). Utafiti huu umekusudiwa kuanza mnamo mwezi wa tisa (September) mpaka mwezi wa kumi(octobar). Utafitihuu utaambatana na kujua wakulima wanataka nini katika maeneo yatakayowahusu.
Katika kuhakikisha mikakati hii ya Muda mfupi inafikiwa kwa kipindi cha muda huu wa mwaka 2013/2014 shirika hadi sasa limefanya yafuatayo.
Kutengeneza vikundi 8 hadi sasa ambavyo vinapatikana katika kata ya Lumesule lakini kusudi la Shirika ni Kuwa na vikundi 21 kwa kata. Hivyo fomu za kujiandikisha kuwa wanavikundi tayari zimesambazwa kwa watendaji wa vijiji kwa watu kujiandikisha na kupewa mafunzo mbalimbali kulingana na mahitaji ya kundi husika. Shirika linatamani kuwa na vikundi vingi zaidi lakini changamoto ya uhakika wa kuwapa mahitaji ndio unaoturudisha nyuma.

Tayari mazungumzo yamefanyika kitaratibu ili serikali za vijiji watuazime ardhi kwa ajili ya Mashamba darasa ambayo yatasaidia kujenga uwezo wa wakulima kwa vitendo baada ya kupewa elimu ya nadharia. Serikali ya Kikiji cha Lumesule imekuwa ya kwanza kukubali ombi hili na michakato infanyika kuhakikisha suala hili linafikia muafaka.
Tayari shirika limeandaaa nyaraka itakayo wezesha kufanya utafiti mdogo (Baseline Survey) kuona ni jambo gani shirika lianze kufanya kazi nalo.
Tayari shirika limeshaunda vikundi vitatu vya kilimo cha bustani toka mwezi wa 4 na sasa wanaendelea na shughuli yao ya kilimo cha bustani chini ya uangalizi wa shirika.

Mikakati ya mda mrefu: (long term strategies)
Kujenga ofisi ya shirika katika kijiji cha lumesule wilayani nanyumbu. Hii ofisi itakuwa makao makuu ya shirika Tanzania nzima huku ikiwa ni pamoja na kujenga ofisi katika kila kanda kulingana na ugaaawanyaji kikanda ikiwa ni katika kanda kuu nne za kanda ya kati, kaskazini, mashariki na kusini.
Kubuni miradi mbalimbali kwa kushirikiana na jamii,serikali pamoja na mashirika ya kimataifa ili kufanikisha  kipato cha mtanzania mmoja mmoja kukua na zaidi kuongea uchumi wanchi,miradi kama ufugaji wa kuku wa kienyeji,kilimo cha mbogamboga,mahindi,ufugaji wa ng’ombe,miradi ya uhakika wa chakula na miradi kupanua na uhakika wa soko la mazao yawakulima.
Kuhamasisha kuhusu swala la elimu mashuleni na zaidi kuunda klabu za kilimo mashuleni na vyuoni ili kumjengea mwanafunzi mbinu mbadala za kukuza kilimo Tanzania kwa kushirikiana na serikali.

MAFANIKIO YA SHIRIKA HADI SASA
Mradi kukubalika na jamii nzima. Mradi umepata nafasi kubwa sana haswa katika eneo ambalo shirika litaweka makao yake makuu wilaya ya nanyumbu na kijiji cha lumesule.Wakionyesha kujawa na furaha wajumbe wengi wamelisifu shirika haswa kuweka makao yake makuu katika mkoa wa mtwara na wilaya ya nanyumbu hasa kata ya Lumesule ambayo mpango wa uhamasishaji umepata ushirikiano mkubwa na mwamko mkubwa sana kutoka kwa jamii husika.


Kuunda vikundi vinane vya wakulima. Baadhi ya vikundi vimewasilisha taarifa zao kuhusu uongozi wao kwa ujumla na uhitaji wao katika kufanya kazi za shirika kitu ambacho kinazidi kulitangaza shirika zaidi


Kufanya vikao pamoja na uongozi wa kijiji cha lumesule ambapo walikubaliana kutoa hekari 10 kwa ajili ya shughuli za shirika.


UZINDUZI WA SHIRIKA NGAZI YA TAIFA, 56 HOTEL MJINI DODOMA KATIKA VIWANJA VYA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA



Uzinduzi wa shirika kitaifa uliofanyikia 56 Hotel Dodoma Tanzania ukihudhuriwa na wageni kama Profesa Mwamfupe kutoka katika chuo kikuu cha Dodoma,Mbunge wa Nanyumbu Mhe.Dastan Mkapa, 
Profesa Davis Mwamfupe, Mshauri wa Wanafunzi katika Skuli ya sayansi za Jamii, katika hotuba yake siku ya uzinduzi wa shirika 16/6/2013 kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao, wizara ya kilimo  Mr Twahil ambaye alimuwakilisha waziri wa kilimo Mh. Eng. Christopher Chiza.
Wengine ni:
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazoa-Wizara ya Kilimo Mr. Twahil
Mkurugenzi wa Mawasiliano na technolojia wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mr. Didas
Mkuu wa idara-Stadi za maendeleo Mrs Mshana
Wakufunzi
Wanataaluma kutoka fani mbalimbali Chuo kikuu cha Dodoma, St john na Mipango


Wadau Mbali mbali wakisikiliza kwa makini maelezo ya shirika la TAFE Mkoani Dodoma.

MIRADI ILIYOBUNIWA NA KUANZA UTEKELEZAJI
Kuanzisha na kusaidia vikundi viwili vya  wakulima wa mbogamboga kijiji cha lumesule;hii ikiwa ni pamoja na kuwapa mbegu hususani katika kilimo cha nyanya;

MRADI WA KARATI…

CHANGAMOTO/ MAHITAJI
Ardhi ya kutosha; kwa sasa na kwa vikao ambavyo shirika limekaa na uongozi a vijiji ni kiasi cha hekari 10 ambazo ziko chini ya shirika mpaka sasa. Lakini ili shirika liweze kufanikisha shughuli zake linahitaji zaidi ya hekari 100. Baadhi ya vikao vilivyokaliwa na uongozi wa vijiji hoja kubwa zilikuwa ni uhitaji wa arthi ya kutosha kufanya shughuli za shirika ziwe rahisi.
Vikundi vya wakulima; tunahitaji vikundi 20 katika kijiji kimoja ambapo mpaka sasa tuna vikundi 8 kwa baadhi ya vijiji. Ili kufanikisha ili ni lazima kuwepo na utafiti tathimini wa wakulima ili kujua wanahitaji nini  na katika mazingira gani.
Kufanyika Kwa utafiti mdogo; ilitarajiwa kuwa utafiti huu ungeanza tarehe 15 mwezi wa nane (August) lakini kutokana na rasilimali pesa kutokukidhi ilimebidi kuahirishwa mpaka mwezi wa tisa (September) mwaka huu.  Mradi wa utafiti mdogo kulingana na mpango kazi utaghalimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi million 17 Tshs (17,000,000 Tshs) ili kufanikisha swala la utafiti mdogo( baseline surveying) Kuhusu hali ya kilo wilayani nanyumbu.
Uhitaji wa miradi mingi kutoka serikalini; shirika linahitaji kuweka ubia na wizara za serikali ili kufanikisha utekelezaji wa shirika na serikali katika kumsaidia mkulima na kuleta maendeleo.
Miradi na utekelezaji; shirika linahitaji ushirikiano mkubwa na halmashauri na wizara chini ya serikali na hivyo uhusiano baina yetu utajegwa na ufanisi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyo chini ya serikali ya maendeleo na kuondoa umaskini (MKUKUTA  na  Tanzania Development Vision 2025) .Pia mashirika yasiyo ya kiserikali yanahitajika ili kujenga uhusiano wa kuisaidia jamii.
Uhitaji wa vifaa mbadala katika kufanikisha shughuli za shirika ikiwemo vifaa vya kisasa vya kuboresha kilimo kama trekta, pump za maji na uchimbaji wamabwawa makubwa ya kuhifadhia maji ili kufanikisha kilimo cha umwagiliaji. Tunaiomba serikali pamoja na wizara zake chini ya  wizara ya kilimo,vijana na maendeleo kutoa ushirikiano kufanikisha ili kwa maendeleo ya wakulima na uimala wa shirika.
Katibu wa shirika alimaliza utambulisho wa shirika kwa kifupi na baadhi ya mikakati,malengo na mahitaji ndani ya shirika kwa sasa na mwenyekiti wa kikao ali mruhusu kupumzika huku akiruhusu michango kutoka kwa wajumbe waliofika katika kikao.
Mjumbe wa almashauri ya kijiji alishukushu uwepo wa shirika katika kijiji cha Lumesule huku akipongeza jitihada za awali za shirika mpaka mahali lilikofika leo hii.”… tunawashurukuru sana shirika la WEZESHA WAKULIMA TANZANIA kwa kuona kilio cha wakulima nchini na haswa katika mkoa wa mtwara zaidi wilaya ya Nanyumbu na pia kijiji cha lumesule… sisi hata mkitaka hekari zaidi ya kumi tutatoa ili shughuli zenu zifanikiwe…” huo ni mchango wa mjumbe kutoka almashauri ya kijiji.
Mjumbe wa pili alisimama na alianza kulipongeza shirika huku akihoji  je kweli shirika litadumu kwa muda katika wilaya ya Nanyumbu,!?
Wajumbe wengine waliosimama walilipongeza shirika kwa uwepo wake huku mmooja wa wajumbe akiwaasa wakulima kwa kusema” …yawezekana hili shirika ni zuri sana lakini likarudishwa nyuma na wakulima wenyewe kwa kutokutoa ushirikiano mbadala na shirika pale wanapohitajika…”

Akilijibu swali la mjumbe kuhusu kuwepo kwa shirika kwa kipindi chote katibu wa shirika alianza kwa kuwaondoa hofu wajumbe wa kikao na kwamba kazi zote za shirika zita fanyika katika ofisi itakayojegwa lumesule na kuwa miradi yote ya shirika ni miradi endelevu itakayoambatana na usimamizi na uhakiki wa miradi (MONITORING AND EVALUATION) na kwa hiyo wakulima wasiwe na wasiwasi kuhusu shirika bali washirikiane kikamilifu ili kufanikisha mahitaji ya shirika.

TAARIFA YA MHE.DASTAN MKAPA, MBUNGE WA JIMBO LA NANYUMBU
Akilizungumzia shirika la TAFE alisema shirika la TAFE ni wanajamii na wanafanya kazi na wakulima. Alisisitiza kuwa shirika ni la wakulima kwani linafanya kazi kwa kuangalia wakulima wanahitaji nini na siyo shirika linahitaji nini.
Mhe Dastan alizidi kuwaasa wakulima kutokuchezea nafasi ya uwepo wa shirika katika wilaya ya nanyumbu bali walisaidie shirika ili kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi kwa kuonyesha ushirikiano pale inapobidi.
Katika taarifa yake fupi mlezi aliahidi…
Kutoa mifuko miwili ya mbolea na dawa kwa ajili ya vikundi viwili vya mbogamboga katika kjiji cha lumesule.
Kushirikiana na shirika pindi litakapoanza kujenga ofisi kwa kutoa mchango wa hali na mali.
Kuzidi kushirikiana katika kulitangaza shirika katika ngazi ya kitaifa ili lifanikisha malengo.

Shirika la wezesha wakulima Tanzania linapenda kuwashukuru jamii kwa kulipokea shirika na zaidi serikali za vijiji kuona umuhimu wa shirika katika kukuza na kuendeleza kilimo Tanzania. Shirika limeeahidi kushirikiana pamoja na wakulima katika maendeleo ya mtanzania.
Ombi letu kwa serikali pamoja na wizara na almashauri kuona umuhimu wa shirika la TAFE mkoani Mtwara na zaidi katika nchi ya Tanzania na hivyo kulisaidia shirika kukua kwa kiwango cha kuletea kipato taifa. Wizara ya kilimo, maendeleo na pia wizara ya vijana inahusiska moja kwa moja katika kufanikisha maendeleo ya mtanzania na hivyo tungeomba wizara hizi kuunga mkono kazi za shirika na zaidi kulisaidia shirika kwani ndio muhimili pekee wa maendeleo ya mtanzania na Tanzania chini ya kilimo. Ili sera ya kilimo isibaki kuwa tu mada bali utekelezaji.


Baadhi ya Wanachama wa TAFE wakiwa katika moja ya sare za shirika katika Majengo ya Chuo Kikuu  Cha Dodoma April 2013.
TAFE MEMBERS

S/N    JINA    NAFASI    MAKAZI    NAMBA YA SIMU      
I    VICTOR WILLIAM    MWENYEKITI    KAGERA    +255752360570      
2    REV.FR.LINUS JOHN    KATIBU MTENDAJI    MTWARA    +255652769009      
3    VICTORIA MPONDA    MHAZINI    RUVUMA    +255757823549      
4    STEVEN NAMAHOCHI    MRATIBU KANDA    MTWARA    +255682674005      
5    BARKA OMARY    MRATIBU KANDA    TANGA    +255713051885      
6    SARAH KAZUMBA    MRATIBU KANDA    MBEYA    +255763541431      
7    JOHN THOMAS    MRATIBU KANDA    ARUSHA    +255769423961      
8    GEORGE MACKONA    AFISA HABARI    DAR ES SALAAM    +255763751879      
9    SHARIFU MUHIBU    MSAIDIZI AFISA HABARI    MTWARA    +255782086830      
10    EDGAR TILYA    MJUMBE     ARUSHA    +255713726156      
11    HALIMA MSITU    MJUMBE    MAFIA    +255715776333      
12     ABUL AZIZ MWASHA    MJUMBE    MANYARA    +255766606592      
13    ABDULATIF AYOUB    MJUMBE    DARES SALAAM    +255653770511      
14    LUIZA HENRY    MJUMBE    MTWARA    +255712247636      
15    AMBROSE JOSEPH    MJUMBE    TARIME    +255752836306      
16    IRENE IBRAHIM    MJUMBE    DAR ES SALAAM    +225713650551      
17    CHARLES SALU    MJUMBE    MWANZA    +255766102783      
18    JOSEPH MWINDOI    MJUMBE    KILIMANJARO    +255757234742      
19     HAPPINESS MSHANA    MJUMBE    MOROGORO    +255658521329   

WANACHAMA WA TAFE NA TAALUMA ZAO.

S/N    JINA    TAALUMA    CHUO      
1    Victor William    Stadi za maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
2    Rev.Fr.Linus John    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
3    Victory Mponda    Stadi za Maendeleo     Chuo kikuu cha Dodoma      
4    John Thomas    Mahusiano ya Kimataifa    Chuo kikuu cha Dodoma      
5    Charles Salu    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
6    Sarah Kazumba    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
7    Barka Omari    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
8    Halima Msitu    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
9    Joseph Ambrose    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
10    Phibert Laurent    General Agriculture     National Sugar institute Morogoro      
11    Joanitha Theophil    General Agriculture    National Institute morogoro      
12    Abdulaziz Ally    Maendeleo vijijini    Chuo Cha Kilimo cha Sokoine       
13    Joseph Muhindoi    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
14    Sharifu Muibu    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
15    Happyness Mshana    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
16    Irene Ibrahim    Stadi za Maendeleo    Chuo Kikuu Cha Dodoma      
17    George Makona    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
18    Luiza Henry    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
19    Abdulaziz Mwasha    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
20    Abdulatif Ayub    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
21    Edger Tillya    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma      
22    Steven Namahochi    Stadi za Maendeleo    Chuo kikuu cha Dodoma   


No comments:

Post a Comment